Mapigano yanaendelea kurindima Kivu Kusini licha ya mkataba wa amani wa Washington

Siku moja baada ya kusainiwa kwa mkataba wa amani kati ya Kinshasa na Kigali nchini Marekani, mapigano mengi yameendelea kurindima mashariki mwa DRC siku ya Ijumaa, Desemba 5. Milipuko kadhaa ilisikika katika maeneo kati ya Bukavu na Uvira, katika jimbo la Kivu Kusini.

Mashariki mwa DRC, mkataba wa amani uliosainiwa siku ya Alhamisi, Desemba 4, huko Washington kati ya marais wa Rwanda na Kongo Paul Kagame na FĂ©lix Tshisekedi, kwa sasa unabaki kuwa ni ndoto tu.

Kulingana na ripoti kadhaa za Umoja wa Mataifa, hasa katika mkoa wa Kivu Kusini, mvutano wa usalama naendelea kuongezeka huko Kaziba na uwanda wa Mto Ruzizi kati ya AFC/M23 inayoungwa mkono na Rwanda na jeshi la Kongo, linaloungwa mkono na wanamgambo wa Wazalendo na jeshi la Burundi. Siku ya Ijumaa, Desemba 5, mashambulizi ya anga yalisababisha vifo vingi na uharibifu mkubwa wa mali.

Mashahidi wameripoti kusikia milipuko mikubwa huko Luvungi na Mutarule, miji miwili iliyoko kati ya Bukavu na Uvira. "Huko Luvungi, raia watatu waliuawa katika kitongoji cha Maendeleo. Wengine watatu pia waliuawa huko Mutarule, ambapo pia kuna watu kadhaa waliojeruhiwa," ammeleza mkazi mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Licha ya mashambulizi ya anga, biashara katika soko la Kamanyola, eneo lililo kwenye mpaka na Rwanda, ziliweza kufunguliwa.

Aliongeza kuwa 90% ya wakazi wa Luvungi walikimbilia vijiji vya jirani na jiji la Uvira. Wengine, walioelekea Burundi, hawakuweza kuingia nchini humo, huku wanajeshi wa Burundi wakipiga kambi kwenye kingo za Mto Ruzizi wakiwazuia kuvuka mpaka.

Wakati AFC/M23, katika taarifa, ikilishutumu jeshi la Burundi kwa kurusha mabomu katika maeneo yenye watu wengi, Bujumbura, nayo, ilimeshutumu kwa kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya eneo lake.

Pia katika eneo hili, biashara katika soko la Kamanyola ziliweza kufunguliwa licha ya milipuko hiyo.

Mapigano mengine pia yameripotiwa mbali kidogo magharibi, kwenye vilima vinavyoelekea kijiji cha Kaziba, katika eneo la Walungu, ambapo wakazi wengi waliokuwa wamejificha katika nyumba zao tangu katikati ya wiki wamehama, anasema mwandishi wa habari kutoka kituo cha redio cha eneo hilo aliyekimbia.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii