Vibali 72 vyatolewa kw a mabasi kuongeza nguvu za safari mwisho wa mwaka

MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imesema mpaka sasa imeshatoa vibali 72 vya kuruhusu wamiliki wa mabasi kuongeza mabasi ya muda ya kusafirisha abiria katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.

Akizungumza kwenye kituo cha mabasi yaendayo mikoani  Mkurugenzi Mkuu wa LATRA Habibu Suluo amesema kuwa  katika kituo hicho cha Magufuli vibali vilivyotolewa mpaka sasa ni 31 na 41 ni katika maeneo mengine ya hapa nchini.

Aidha amesema kuwa wamefanya hivyo kutokana na idadi kubwa ya abiria wanaosafiri katika kipindi hiki kwenda kwenye mapumziko ya mwisho wa mwaka kwenye mikoa mbalimbali nchini. 

Kadhalika akiwa kituoni hapo alfajiri baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kufanya ukaguzi na kuangalia hali ya usafiri, Suluo amesema amebaini kuwapo kwa udanganyifu kwa baadhi ya mawakala wa mabasi ambao baadhi yao walikamatwa na Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Amesema udanganyifu ambao amebaini ni kuwapo kwa baadhi ya mawakala hao ambao wanawatoza abiria nauli zaidi ya ile iliyowekwa na Mamlaka hiyo.

Pia, amesema baadhi ya mawakala walibainika kutengeneza tiketi feki za karatasi ambazo nyingine wamezitoa kopi na kuwauzia abiria wakiwaandikia magari ambayo mengine hayapo na ameeleza kuwa wamebaini baadhi ya magari kutumia wahudumu ambao hawajasajiliwa na LATRA.

Hata hivyo  Mamlaka hiyo inaendelea ukaguzi na kwamba itaendelea kuchukua hatua kwa wale wote wanaokiuka sheria na taratibu za usafirishaji.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii