Nigeria yawezesha kuachiwa huru wanafunzi 100 waliotekwa

Serikali ya Nigeria imewezesha mpango wa kuachiliwa huru kwa wanafunzi 100 waliotekwa nyara na watu wenye silaha katika shule ya Kikatoliki mwezi uliopita.

 Hayo yameelezwa siku ya Jumapili na chanzo kimoja cha Umoja wa Mataifa ikiwa Wanafunzi hao wamewasili mjini Abuja na kukabidhiwa kwa viongozi wa utawala ambapo mpango huo ulifikiwa kupitia mazungumzo au nguvu za kijeshi huku hatima ya wanafunzi wengine 165 na wafanyakazi kadhaa waliotekwa ikiwa bado haijulikani.

Hata hivyo mwishoni mwa mwezi Novemba wanafunzi 315 na wafanyakazi walitekwa nyara kutoka shule ya bweni ya Mtakatifu Maria iliyoko kaskazini mwa jimbo la Niger takriban wanafunzi 50 walitoroka muda mfupi baadaye. Makundi yenye silaha nchini  Nigeria  yamekuwa yakiwateka watu na kudai kikomboleo kama njia ya kujipatia fedha kwa haraka.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii