Mapigano makali yameendelea kushuhudiwa huko Uvira mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambapo waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda kwa kukabiliana na jeshi la Kongo linaloungwa mkono na wanajeshi wa Burundi.
Shirika la Msalaba Mwekundu limesema kuwa raia wapatao 20 wakiwemo watoto wamejeruhiwa huku wanajeshi 20 wa Burundi wameripotiwa kuuawa kwenye mapigano hayo tangu yalipozuka upya Jumatatu iliyopita.
Hata hivyo vyanzo kadhaa vya kijeshi vimeeleza kuwa kwa sasa wanajeshi wa Burundi wamewadhibiti waasi wa M23 na kuwasababishia pia hasara.
Itakumbukwa kuwa pande zote mbili zinapigania udhibiti wa mji wa DRC wa Kamanyola ambao unapakana na mataifa ya Rwanda na Burundi na ambao kwa sasa unadhibitiwa na M23 ambapo mapigano hayo yanaripotiwa ikiwa ni siku chache tu baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya amani kati ya rais wa Rwanda Paul Kagame na mwenzake wa DRC Felix Tshisekedi mjini Washington.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime