Syria Jumatatu inaadhimisha mwaka mmoja tangu kuangushwa kwa mtawala wa kidikteta Bashar al Assad, wakati taifa hilo lililoganwanyika likapambana kurejesha utulivu na kujijenga upya baada ya vita vya muda mrefu.
Rais wa mpito Ahmed al-Sharaa aliyefanikiwa kuongoza harakati za mapinduzi na kuuhitimisha utawala wa Bashar ameongoza maadhimisho hayo kwa sala ya alfajiri katika msikiti wa Umayyad, mjini Damascus, hii ikiwa ni kulingana na shirika la habari la SANA.
Assad alikimbilia Urusi mwaka uliopita kufuatia mapinduzi hayo ambayo pia yalihitimisha vita vya zaidi ya miaka 13 vilivyotokana na uasi dhidi yake.
Kulingana na SANA, Sharaa, kamanda wa zamani wa kundi la kigaidi la al-Qaeda ameahidi kuijenga Syria tena ya haki na imara na miundo itakayoendana na nyakati za sasa na zilizopita.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime