Jenista Mhagama afariki dunia

Mbunge wa Peramiho Jenista Joakim Mhagama amefariki dunia leo 11 Desemba mwaka huu jijini Dodoma.

Taarifa hiyo imetolewa na Spika wa Bunge la Tanzania Mussa Azzan Zungu ambaye ameeleza kuwa Bunge limepokea msiba huo kwa masikitiko makubwa.

Hata hivyo Spika ametuma salamu za pole kwa Wabunge, familia, ndugu, jamaa pamoja na wananchi wa Jimbo la Peramiho kwa  kumwomba Mungu awape nguvu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu na kusema mipango ya mazishi itatolewa na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii