Waziri Ulega awasili Mwanza kutekeleza agizo la PM ukaguzi wa madaraja

Waziri wa Ujenzi Mhe. Abdallah Ulega (MB) leo Desemba 11 mwaka huu amefika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na kufanya mazungumzo mafupi na Mhe. Mtanda na kubainisha kuwa yupo kwenye ziara ya siku moja mkoani humo ya kukagua utekelezaji wa ujenzi wa madaraja ya Mkuyuni na Mabatini.

Mhe. Ulega amesema ujenzi wa madaraja hayo yaliyopo katikati ya Jiji la Mwanza ni muhimu sana kwani ndio kiunganishi cha kuingia na kutoka mjini hivyo atakutana na wakandarasi na kuwekeana mikakati ya ukamilishaji.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amemwambia Mhe Ulega kwamba baada ya ziara ya Mhe Waziri Mkuu kuwa alikutana na wakandarasi wanaojenga madaraja hayo na wakawekeana mpango kazi wa ukamilishaji kwa haraka ambao ndio sasa wanaufuata.

Aidha Mhe. Mtanda ametoa rai kwa wizara ya Ujenzi kukiondosha kivuko kimoja kilichobaki katika gati la Kigongo hata baada ya kukamilika kwa daraja la JP Magufuli ili kikasaidie kutoa huduma ya kuvusha abiria katika visiwa ambavyo vinauhitaji wa usafiri wa majini.

Waziri Mkuu alifanya ziara Mkoani Mwanza hivi karibuni na kubaini adha wanayoipata wananachi kutokana na daraja la Mkuyuni linalotekelezwa na mkandarasi Jasco building and civil contractors (5.7 B) na daraja la Mabatini linalotekelezwa na Nyanza Road Works Ltd (6 B) kuchelewa kukamilika ndipo akamtaka Waziri wa ujenzi kufika mara moja kukagua utekelezaji.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii