Hamas yashtumiwa kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limetoa ripoti yake inayolishutumu kundi la Hamas na makundi mengine ya wapiganaji wa Kipalestina kwa kufanya uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Katika ripoti yake ya kurasa 173 Amnesty International imesema makundi ya wapiganaji wa Kipalestina yalikiuka sheria za kimataifa za kibinadamu na kufanya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu wakati wa shambulizi kusini mwa Israel mnamo Oktoba 7 mwaka 2023.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa Hamas na makundi mengine ya wapiganaji wa Kipalestina "yaliendelea kufanya uhalifu na kukiuka sheria za kimataifa kwa kuwachukua watu mateka na kuwatesa, pamoja na kuzuia miili ya watu waliotekwa."

Amnesty International pia imeishtumu Israel kwa kufanya mauaji ya kimbari wakati wa kampeni yake ya kijeshi katika ukanda wa Gaza - shutma ambayo serikali ya Israel imekanusha vikali.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii