Baadhi ya vyombo vya habari vimeonyesha waasi wa M23 wakiingia Uvira na kudhibiti maeneo muhimu ya mji huo ikiwemo ofisi za serikali na maeneo ya mpakani.
Kundi la waasi la M23 linaloungwa mkono na Rwanda limetangaza kwamba limechukua udhibiti wa mji wa Uvira, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Tangazo hilo, lililotolewa kupitia mtandao wa kijamii wa X na msemaji wa kundi hilo Lawrence Kanyuka, limewahimiza wakazi waliokimbia kurejea makwao.
Uvira ni mji wa bandari muhimu ulioko kaskazini mwa Ziwa Tanganyika, mkabala na mji mkuu wa Burundi, Bujumbura.
Mashambulizi ya hivi karibuni ya waasi wa M23 yametokea licha ya makubaliano ya amani yaliyosimamiwa na Marekani na kutiwa saini wiki iliyopita mjini Washington na Rais wa Kongo Félix Tshisekedi na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime