Aliyewahi kuwa Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Peramiho, Jenista Joakim Mhagama, aliyefariki dunia Desemba 11 mwaka huu jijini Dodoma, anatarajiwa kuzikwa Desemba 16 mwaka huu Ruanda – Mbinga.
DESEMBA 12, 2025
Mwili wa Marehemu utaletwa nyumbani kwake Itega, Dodoma kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho.
DESEMBA 13, 2025
Misa Takatifu itafanyika katika Parokia ya Kiwanja cha Ndege, Dodoma.
Baada ya misa, mwili utasafirishwa kuelekea Songea.
DESEMBA 14, 2025
Kuwasili Songea.
Maombolezo yataendelea, ikifuatiwa na Misa na mwili kupumzika nyumbani kwake Makambi.
DESEMBA 15, 2025
Safari ya kuelekea Peramiho.
Misa Takatifu, kutoa heshima za mwisho, na mwili kulala Peramiho.
DESEMBA 16, 2025
Mazishi yatakayofanyika Ruanda, Mbinga.
