Umoja wa Ulaya katika taarifa kwa vyombo vya habari mapema wiki hii ulitangaza kutoa karibia Euro Milioni 10 kwa FARDC kabla ya mwisho wa mwaka ujao kuboresha operesheni ya jeshi la DRC
Ufadhili huo utakwenda moja kwa moja kwa jeshi la Kongo kulisaidia kupata vifaa ili kuimarisha uwezo wake wa kufanya kazi. Vifaa hivi vitajumuisha zana za mawasiliano,kuboresha operesheni, vifaa vya matibabu pamoja na vifaa vya kuwezesha jeshi hilo kushika doria kwenye mipaka na mito.
Uwasilishaji wa kwanza umepangwa kufanyika ya kabla ya mwisho wa 2026.
Hii ni awamu ya pili ya ufadhili kutolewa kwa FARDC kutoka Umoja wa Ulaya.
Awamu ya kwanza, iliyotolewa mwaka wa 2023, ililenga kusaidia kikosi cha 31 kilichoko eneo la Kindu.
Kutokana na msaada huu sasa jumla ya missada kutoka kwa mfumo wa amani wa Ulaya kwa FARDC umefikia Euro Milioni 30.
Msaada huu ni sehemu ya juhudi za Umoja wa Ulaya kuimarisha mageuzi ya sekta ya usalama nchini DRC na kuunga mkono FARDC katika oparesheni zake kulinda raia na kurejesha mamlaka ya serikali, huku ikichangia mchakato wa amani.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime