Jeshi la Sudan lasema limezuia shambulizi la RSF

Jeshi la Sudan limesema limezuia shambulizi la wanamgambo wa RSF kwenye mji muhimu kusini mwa nchi hiyo jana Jumanne, huku Marekani ikizihimiza pande zote mbili kukubali pendekezo la kusitisha mapigano.

Jeshi hilo lilizuia shambulizi kwenye kambi yake katika mji wa kimkakati wa Babanusa ambao ni ngome yake kubwa ya mwisho katika eneo hilo.

Babanusa iko kwenye njia muhimu ya usafirishaji kati ya mji mkuu Khartoum kupitia Kordofan na Darfur.

Mapema jana, mjumbe wa Marekani barani Afrika, Massad Boulos alisema akiwa Abu Dhabi kwamba pande zote hazijakubaliana na pendekezo jipya la kusitisha mapigano lililoandaliwa na kundi la Quad linalojumuisha Marekani, Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu na Misri.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii