Wakati nchi za Rwanda na DR Congo zikitarajiwa kutia saini wiki hii makubaliano ya amani jijini Washington Marekani, Kigali na Kinshasa zimeendelea kutuhumiana kuhusu mzozo wa mashariki ya Kongo.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Kongo, anasisitiza kwa jamii ya kimataifa kuiwekea vikwazo Rwanda kutokana na kuendelea kuwaunga mkono waasi wa M23 mashariki ya Kongo, madai ambayo yamekanishwa vikali na mwenzake wa Rwanda.
Kigali inasema uongozi wa Kinshasa umefeli katika suala la uongozi na kwamba unatupia lawama jirani zake.
Madai ya sasa yanaonekana kurudisha nyuma hatua na juhudi zinazopigwa kumaliza mzozo uliopo, zikiwemo za kidiplomasia, huku mpango wa utekelezwaji wa makubalianoa ya amani ukikabiliwa na sintofahamu.
Kwa mujibu wa Serikali zote mbili, rais wa Rwanda, Paul Kagame na mwenzake wa DRC, Felix Tschisekedi, juma hili watasafiri Kwenda Washington tayari kwa kutia Saini mkataba huo ambao ikiwa utaheshimiwa utamaliza vita mashariki mwa kongo.
Kando na mapigano yanayoendelea mashariki mwa Congo, wiki iliopita, Rais wa Rwanda Paul Kagame aliuutuhumu utawala wa Kinshasa kwa kuchelewesha kwa makusudi utekelezwaji wa makubaliano ya amani.
Aidha licha ya kwamba Rais wa Kongo Felix Tshisekedi amekubali kushiriki kikao cha utiaji saini makubaliano haya tarehe 4 ya mwezi huu jijini Washington, mwenzake Paul Kagame, bado hajathibitisha.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime