Viongozi wa Umoja wa Ulaya hatimaye wamefikia makubaliano ya kuipatia Ukraine mkopo wa kiasi cha yuro bilioni 90 katika kipindi cha miaka miwili ijayo, hii ikiwa ni kulingana na Rais wa Baraza la Ulaya.
Katika taarifi aliyoiandika Antonio Costa kupitia mtandao wa X huku akithibitisha juu ya uamuzi huo na kwamba fedha hizo zitatumia kwa mwaka 2026 hadi 2027.
Aidha Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz amesema mapema leo Ijumaa kwamba Umoja wa Ulaya umetuma "ishara ya wazi" kwa kiongozi wa Urusi Vladimir Putin, kufuatia makubaliano hayo.
Hata hivyo ameandika kupitia mtandao wa X kwamba, huo ni ujumbe kwa Putin kwamba, Vita vyake nchini Ukraine havitakuwa na maana tena.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime