Wanaume saba wanaoaminika kuwa na uhusiano wa kiitikadi na washambuliaji wawili waliohusika na shambulizi la kigaidi kwenye ufuo wa Bondi siku ya Jumapili wamekamatwa kusini-magharibi mwa Sydney.
Taarifa hiyo imetolewa na kituo vyombo habari nchini Australia siku ya Ijumaa ambao polisi wa New South Wales wamewakamata wanaume hao katika kitongoji cha Liverpool huko Sydney jana Alhamisi, wakitokea jimbo jirani la Victoria wakitumia magari mawili.
Aidha Naibu Kamishna wa Polisi wa NSW David Hudson aliviambia vyombo vya habari kwamba kulikuwa na "ishara fulani kwamba Bondi lilikuwa ni moja ya maeneo ambayo huenda waliyatembelea.
Hata hivyo Waziri mkuu wa Australia mapema leo ametangaza mpango wa kitaifa wa kununua tena bunduki ili kuziondoa silaha nzito kufuatia mauaji hayo yaliwaua watu 15 na kuwajeruhi wengine kadhaa.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime