Marekani yawawekea vikwazo majaji wawili zaidi wa ICC

Serikali ya Marekani imewawekea vikwazo majaji wawili zaidi wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kutokana na uchunguzi wake dhidi ya raia wa Israel.

Majaji hao walioongezwa kwenye orodha ya vikwazo ni Erdenebalsuren Damdin wa Mongolia na Gocha Lordkipanidze wa Georgia, imesema taarifa ya Wizara ya Fedha.

Marekani kupitia Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio imesema ICC imeendelea kujihusisha na vitendo vya kisiasa vinavyoilenga Israel, na ambavyo vimeonyesha mfano mbaya mbele ya mataifa yote.

Serikali hiyo imeishutumu mahakama hiyo kwa "matumizi mabaya ya madaraka" yanayokiuka uhuru wa Marekani na mshirika wake wa karibu Israel ambapo serikali ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameukaribisha uamuzi huo.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii