Rais wa zamani wa Iraq awa mkuu mpya wa UNHCR

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Alhamisi lilimuidhinisha Rais wa zamani wa Iraq Barham Salih kuwa mkuu ajaye wa shirika la wakimbizi, UNHCR, akiwa ni kwanza kutoka Mashariki ya Kati tangu mwishoni mwa miaka ya 1970.

Baraza hilo lenye wanachama 193 lilimchagua mwanasiasa huyo wa Kikurdi mwenye umri wa miaka 65 kuwa kamishna mkuu wa UNHCR kwa makubaliano na Rais wa Baraza Kuu Annalena Baerbock.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amemsifu kiongozi huyo kutokana na uzoefu wake kwenye eneo la diplomasia, siasa na utawala na kumtaja kama mbunifu wa mageuzi ya kitaifa.

Salih anachukua nafasi ya Filippo Grandiambaye muda wake wa awamu ya pili unamalizika Disemba 31 mwaka huu Kipindi cha Salih kitaanza Januari Mosi.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii