Maandamano yaliyoambatana na vurugu yamezuka kote mjini Dhaka na sehemu nyingine za Bangladesh kufuatia kifo cha mwanaharakati maarufu Sharif Osman Hadi kutangazwa Alhamisi jioni.
Waandamanaji hao wanashinikiza wauaji wa mwanaharakati huyo aliefia katika hospitali ya Singapore jana desemba 17 mwaka huu kukamatwa.
Hata hivyo mwanaharakati huyo alifariki wakati akitibiwa baada ya kupigwa risasi kichwani mnamo Desemba 12 mwaka huu na mtu aliyekuwa kwenye pikipiki na aliyevalia barakoa.
aidha itakumbukwa kuwa mwanaharakati huyo alikuwa mmoja ya watu mashuhuri zaidi wakati wa uasi wa 2024 uliokomesha utawala wa kidikteta waWaziri Mkuu wa zamani Sheikh Hasina, aliyekimbilia India.