Jumla ya watu milioni 6.8 katika taifa hilo la Afrika Magharibi wanatarajiwa kujitokeza siku ya Jumapili majira ya 7:00 asubuhi hadi saa 6:00 jioni kuwapigia kura wagombea tisa wa nafasi ya urais.
Wagombea hao wa urais nchini Guinea akiwemo kiongozi wa kijeshi nchini humo Jenerali Mamady Doumbouya wamefanya mikutano yao ya mwisho ya kampeni za kisiasa hapo jana kabla ya uchaguzi mkuu mwishoni mwa juma.
Jumla ya watu milioni 6.8 katika taifa hilo la Afrika Magharibi wanatarajiwa kujitokeza siku ya Jumapili majira ya 7:00 asubuhi hadi saa 6:00 jioni kwa saa za Afrika Magharibi kuwapigia kura wagombea tisa wa nafasi ya urais akiwemo Doumbouya mwenyewe mwenye miaka 41 na ambaye ni mgombea huru.
Licha ya ahadi yake ya awali ya kurudisha mamlaka kwa raia alipochukua hatamu mwaka 2021, Doumbouya anagombea urais katika uchaguzi ambao upinzani wote mkuu umezuiwa.
Itakumbukwa kwamba tangu uhuru wake mwaka 1958, Guinea imekuwa na historia tata ya utawala wa kijeshi na kimabavu.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime