Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia, Najib Razak, amehukumiwa tena Ijumaa kwa makosa ya ufisadi yanayohusiana na uporaji wa mabilioni ya dola kutoka mfuko wa uwekezaji wa taifa, 1MDB.
Mahakama Kuu ya Malaysia ilimpata na hatia kwa makosa manne ya matumizi mabaya ya madaraka, huku hukumu za ziada za utakatishaji fedha zikiendelea kutolewa.
Mamlaka zinasema Najib alihamisha zaidi ya dola milioni 700 kwenye akaunti zake binafsi kutoka mfuko wa 1MDB, madai ambayo ameyakana akisema fedha hizo zilikuwa mchango wa kisiasa kutoka Saudi Arabia.
Najib, aliyekuwa Waziri Mkuu kati ya 2009 na 2018, tayari anatumikia kifungo cha miaka 12 gerezani baada ya hukumu ya awali mwaka 2020 kwa makosa yanayohusiana na 1MDB.
Najib, ambaye alionekana kuwa asiyeweza kuguswa kwa muda mrefu, alikabili hasira ya umma iliyopelekea chama chake kushindwa katika uchaguzi wa 2018.
Hivi karibuni, ombi lake la kutumikia kifungo nyumbani lilikataliwa na Mahakama KuuKwa sasa, Najib anatarajiwa kuendelea gerezani kwa muda mrefu zaidi, huku mke wake Rosmah Mansor naye akikabili hukumu ya miaka 10 gerezani kwa kesi tofauti ya ufisadi.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime