Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasili katika Shule ya Kijeshi ya Ulinzi wa Anga (SKUA) mkoani Tanga leo Desemba 15 mwaka huu kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano wa 9 wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Makamanda.
Mkutano huu unalenga kuimarisha ushirikiano wa kijeshi kuboresha mikakati ya ulinzi wa taifa, na kuchambua changamoto na mafanikio ya jeshi katika kuhakikisha usalama wa nchi na raia wake.
Rais Samia amekuwa mstari wa mbele katika kuhimiza ufanisi na uwajibikaji katika majeshi, huku akisisitiza umuhimu wa kuendeleza mafunzo bora, ujasiri na nidhamu miongoni mwa maofisa na askari wa Tanzania.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime