Elon Musk mmiliki wa jukwaa la X (zamani Twitter) ametambulisha rasmi XChat mfumo mpya wa mawasiliano ulioundwa kuboresha faragha na kuongeza kasi ya uhuru wa mazungumzo ya kidijitali.
Hivyo basi XChat imejengwa kwa teknolojia ya kisasa ikiwa na usanifu wa lugha ya Rust na kutumia mbinu za usalama zinazofanana na zile za Bitcoin kwa lengo la kuimarisha faragha na kuzuia udukuzi wa taarifa za watumiaji.
Huduma Kuu za XChat
Usalama wa End-to-End Encryption: Ujumbe unasomwa tu na mtumaji na mpokeaji.
Ujumbe Unaofutika (Disappearing Messages): Ujumbe huondolewa baada ya muda maalumu.
Simu za Sauti na Video: Bila kuhitaji namba ya simu.
Kutuma Mafaili Bila Mipaka: Rahisi kwa watumiaji kushiriki taarifa kubwa.
Tofauti na majukwaa mengine ya mawasiliano XChat inalenga kuwapa watumiaji uhuru zaidi, udhibiti kamili wa data zao, na faragha ya hali ya juu, hasa kwa wale wanaopendelea mawasiliano bila kuunganishwa na namba ya simu.
Wataalamu wa teknolojia wanaona XChat kama zaidi ya app ya kawaida ya chat, bali sehemu ya mkakati mpana wa Elon Musk wa kuifanya X kuwa “everything app” jukwaa linalojumuisha mawasiliano, biashara, na huduma mbalimbali za kidijitali.
Hata hivyo wachambuzi wamesema bado kuna haja ya uhakiki zaidi wa kiufundi ili kuthibitisha kiwango kamili cha usalama, hasa katika masuala ya data na metadata.
Kwa sasa XChat inaendelea kutolewa kwa awamu kwa watumiaji wa jukwaa la X, huku ikitarajiwa kupanuka zaidi siku zijazo.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime