Hizi hapa baadhi ya sababu Zinazopelekea Gari la Rais wa Marekani kuogopwa zaidi Duniani

Rais wa Marekani Donald Trump ni kiongozi wa taifa lenye nguvu kubwa zaidi kisiasa, kiuchumi na kijeshi duniani hivyo basi katika nafasi hiyo nyeti, usalama wake hupewa kipaumbele cha juu kabisa na ndiyo maana katika kila safari ya tukio rasmi au ziara ya kimataifa, Rais husafiri ndani ya gari maalum linalojulikana kwa jina la “The Beast”, au Cadillac One gari ambalo limeundwa mahsusi kumlinda Rais kwa kiwango cha juu kuliko gari lolote duniani.

 Ingawa '' The Beast; Kwa muonekano wa nje pamoja na '' Cadillac One ''yanaonekana kama magari ya kifahari ya kawaida sana kama Cadillac hata hivyo ndani yake kuna teknolojia nzito za ulinzi zinazoyafanya magari hayo kuwa ngome kamili inayotembea Mwili wake umetengenezwa kwa chuma maalum chenye uwezo wa kuhimili risasi kali na milipuko huku madirisha yakiwa ni glasi nene zisizopenyeka kwa urahisi.

Teknolojia za Usalama wa Kipekee

Usalama wa Rais hauishii kwenye chuma pekee The Beast lina vifaa vya kisasa vinavyolifanya liwe tayari kwa hali yoyote:

  • Mfumo wa hewa safi wa dharura, endapo kutatokea shambulio la kemikali au gesi hatarishi

  • Akiba ya damu ya Rais, inayolingana na kundi lake la damu kwa matumizi ya haraka

  • Matairi ya run-flat yanayoweza kuendelea na safari hata yakilipuliwa

  • Mawasiliano ya siri ya moja kwa moja na vyombo vya ulinzi vya Marekani

    Nguvu na Utendaji wa Hali ya Juu

    Licha ya uzito wake mkubwa unaotokana na ulinzi mzito, The Beast lina injini yenye nguvu kubwa inayoliwezesha kusafiri kwa uthabiti na kasi inapohitajika. Hii humhakikishia Rais usalama na ufanisi katika safari zake, hata katika mazingira yenye hatari.

    Alama ya Mamlaka na Heshima ya Taifa

    Aidha Cadillac One si gari la kawaida itabakia kuwa  nembo ya mamlaka ya Rais wa Marekani. Linapoonekana barabarani, linaashiria uwepo wa kiongozi wa taifa kubwa duniani, pamoja na uwezo wa teknolojia na mfumo wa ulinzi wa Marekani.

    #10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii