Trump aishitaki BBC akitaka fidia ya dola bilioni 10

Rais Donald Trump wa Marekani amefunguwa kesi mahakamani akidai fidia ya dola bilioni 10 kutoka Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC, akilituhumu kumchafulia jina.

Kesi hiyo inatokana na vipande vya video vilivyohaririwa vya hotuba yake aliyoitowa tarehe 6 Januari 2021, inayotajwa kuchochea uvamizi uliofanywa na wafuasi wake dhidi ya bunge.

Ingawa tayari BBC  ilishakiri na kuomba radhi kwa suala hilo ambapo mawakili hapo jana waliiambia mahakama kuu mjini Miami, kwamba shirika hilo la utangazaji halijaonesha kujuta kweli wala kufanya mabadiliko yoyote yanayoweza kuzuwia hali kama hiyo isijitokeze tena.

Aidha Msemaji wa BBC ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba hawana tena mawasiliano na mawakili wa Trump na kwamba msimamo wao unasalia kuwa ule ule.

Hata hivyo Machafuko yaliyotokana na uvamizi huo wa Bunge la Marekani yalisababishwa na Trump kupinga matokeo ya uchaguzi ambayo alishindwa na hasimu wake, Joe Biden wa Democrat.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii