Mshirika wa Embalo akamatwa na euro milioni 5 taslim

Mshirika wa karibu wa rais aliyepinduliwa nchini Guinea Bissau, Umar Sissoco Embalo ametiwa nguvuni nchini Ureno akiwa na kiasi cha fedha taslimu euro milioni tano.

Hata hivyo Mtu huyo alishikiliwa kwenye uwanja wa ndege wa kijeshi wa Figo Maduro siku ya Jumapili (Disemba 14) lakini akaachiwa kwa dhamana siku ya Jumatatu, kwa kuwa chini ya sheria za Ureno, adhabu ya kosa alilokamatiwa haizidi kifungo cha miaka mitano jela.

Kufuatia taarifa hiyo Fedha hizo ambazo ni sawa na takribani dola milioni sita za Kimarekani zilikamatwa ikiwa ni wiki tatu tu tangu mapinduzi ya kijeshi kwenye taifa hilo la pwani ya Afrika Magharibi.

Aidha idara ya Mwendesha Mashitaka haikuweka hadharani jina la mshukiwa huyo ingawa vyombo vya habari vya Ureno vimemtaja kama mpambe wa Embalo na kwamba alikamatwa akiwa kwenye ndege moja na mke wa rais huyo wa zamani, ingawa mke huyo hakutiwa kizuizini.

Itakumbukwa kuwa Embalo alipinduliwa na jeshi baada ya uchaguzi wa mwishoni mwa mwezi Novemba ambapo upinzani wake ulidai kuwa ulishinda.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii