Rais wa Kenya William Ruto amemteua Truphena Muthoni kuwa balozi wa kampeni ya taifa ya kupanda miti, kufuatia jitihada zake za kipekee katika kulinda na kuhamasisha uhifadhi wa mazingira.
Akizungumza Desemba 15 mwaka huu wakati wa kumpokea Ikulu Rais Ruto alisema hatua ya Muthoni imekuwa mfano wa kuigwa huku akisisitiza kuwa jitihada za mtu mmoja zinaweza kuamsha dhamira ya taifa zima katika kulinda mazingira.
Hata hivyo uteuzi huo unakuja siku chache baada ya Muthoni (22) kuweka rekodi ya kukumbatia mti kwa muda wa siku tatu mfululizo (saa 72) bila kula wala kulala akitaja mapenzi yake juu ya umuhimu wa kutunza miti katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime