Watu 30 washitakiwa kwa jaribio la mapinduzi Benin

Mahakama ya Uhalifu wa Kiuchumi na Ugaidi nchini Benin imewashitaki watu wapatao 30 ambao wengi wao wakiwa ni wanajeshi kwa jaribio la mapinduzi lililoshindwa mapema mwezi juu.

Katika taarifa iliyotolewa na vyanzo mbalimbali vya habari ambavyo vimebainisha kuwa mahakama imewatia kizuizini washtakiwa hao  kwa kosa la uhalifu, mauaji na kuhatarisha usalama wa taifa.

Aidha Wanajeshi wa ngazi za chini walijitokeza kwenye televisheni ya taifa hilo la Afrika Magharibi mnamo Disemba 7 mwaka huu na kutangaza kumpinduwa Rais Patrice Talon  ingawa  jaribio hilo lilizimwa kwa haraka na wanajeshi watiifu kwa msaada wa kikosi cha anga cha Nigeria na kikosi maalum cha Ufaransa.

Hata hivyo licha ya kusifika kwa kuchochea ukuaji wa uchumi Rais Talon anatuhumiwa na wakosoaji wake kwa udikteta katika taifa hilo lililowahi kutajwa kuwa mojawapo ya alama za demokrasia ambapo watu kadhaa waliuawa na hadi sasa kiongozi wa jaribio hilo Luteni Kanali Pascal Tigri na wanajeshi wengine walioasi hawajapatikana.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii