M23 wajiondowa Uvira kwa agizo la Marekani

Imefahamika kuwa kujiondowa kwa kundi la waasi wa M23 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutoka mji muhimu wa Uvira kumetokana na agizo la Washington.

katika taarifa iliyotelawa nchini humo emeelezwa kuwa Marekani iliapa kulichukulia  hatua kali  kundi hilo kutokana na "uvunjaji wa wazi wa mkataba wa amani" uliosimamiwa na Ikulu ya White House.

Aidha kundi hilo linaloungwa mkono na Rwanda lilichukuwa udhibiti wa mji huo wa kimkakati karibu na mpaka wa Burundi wiki iliyopita, siku chache baada ya serikali za Kongo na Rwanda kusaidi mkataba wa amani mjini Washington, mkataba ambao Rais Donald Trump aliusifia kuwa "muujiza mkubwa."

Hatua hiyo ya M23  imeutia doa mchakato huo wa amani na kuzusha hofu za vita vikubwa zaidi vya kikanda  ambapo kuushikilia kwake mji wa Uvira uliliwezesha kundi hilo kudhibiti mpaka wa Kongo na Burundi na kuikatia serikali mjini Kinshasa msaada wa kijeshi kutoka jirani yake huyo.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii