Venezuela imetuma malalamiko yake rasmi kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya kile inachokiita "wizi" wa Marekani iliyoiteka meli yake ya mafuta kwenye Bahari ya Karibiani wiki iliyopita.
Hivyo kwa mujibu wa barua ya wizara ya mambo ya kigeni ya Venezuela iliyochapishwa jana huko Caracas kwa kuutaka Umoja wa Mataifa kulaani uharamia huo unaofanywa na Marekani juu ya matumizi ya nguvu za kijeshi yasiyo halali dhidi ya vyombo vya baharini na wizi wa mzigo ulio kwenye safari halali kimataifa.
Aidha Venezuela imetaka pia kuachiliwa mara moja kwa mabaharia wake wanaoshikiliwa na Marekani. Barua hiyo iliwasilishwa kwa rais wa sasa wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, mwanadiplomasia Samuel Zbogar wa Slovenia.
Hata hivyo Rais Nicolas Maduro wa Venezuela amedai kuwa hatua ya Marekani kutuma kiwango kikubwa cha wanajeshi karibu sana na nchi yake ni sehemu ya mpango wa kumuondowa madarakani na kuiba akiba kubwa ya mafuta kwa kisingizio cha vita dhidi ya madawa ya kulevya.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime