Mataifa ya Ulaya yaanzisha Kamisheni ya Madai ya Ukraine

Baraza la Ulaya ni shirika linaloongoza kwa masuala ya haki za binaadamu barani humuna na pia limepiga hatua muhimu kuelekea ulipaji wa fidia za kivita kwa watu wa Ukraine.

Hatua hiyo imepelekea Baraza hilo lilikubaliana mjini The Hague na Uholanzi mnamo Disemba 16 mwaka huu kuanzisha kile kinachoitwa Kamisheni ya Kimataifa ya Madai kama sehemu ya mfumo wa fidia.

Aidha katika makubaliano hayo yaliyohudhuriwa na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky  aliwashukuru washiriki kwa uungaji mkono wao kwa nchi yake kwa kuanzisha kamisheni hiyo maalum  iliyosainiwa na mataifa 34, ikiwemo Ujerumani na pia Umoja wa Ulaya  na mashirika yaliyo nje ya Ulaya yanaweza pia kujiunga na mpango huo kwa mujibu wa makubaliano hayo.

Hata hivyo Kamisheni hiyo imepewa jukumu la kutathmini madai ya fidia kutoka kwa raia wa kawaida, jumuiya na mashirika ya umma yaliyoathirika na uvunjaji wa sheria za kimataifa uliofanywa na Urusi, na kisha kuamua kiwango cha fidia kinachopaswa kulipwa.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AAhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii