Madumu ya mafuta ya magendo yakamatwa Ubungo

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekamata madumu 23,755 ya mafuta ya kupikia yaliyoingizwa nchini Tanzania kinyume na taratibu kupitia Bandari ya Kunduchi jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Kamishna Mkuu wa TRA Yusuph Mwenda baada ya kukagua mzigo huo Desemba 16 mwaka huu katika eneo la magofu Ubungo ulipokuwa umefichwa amewataka wananchi kufuata taratibu zinazotakiwa wanapotaka kuingiza bidhaa kwani kutokufanya hivyo kunaathiri uchumi wa taifa.

Mafuta hayo yalikamatwa baada ya wasamaria wema kutoa taarifa kwa TRA juu ya kuingizwa kwa mzigo huo kinyume na taratibu huku ukaguzi wa awali ukionyesha kuwa madumu 5,000 pekee ndiyo yalikuwa na nyaraka.

Aidha Mbali na kuwa na athari katika uchumi pia bidhaa zisizopitia ukaguzi wa mamlaka husika huweza kuwa hatari kwa afya za walaji  hivyo ni wajibu wa kila mmoja kushiriki katika kuzuia biashara hiyo haramu.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii