Wafahamu wanawake watano Afghanistan waliokataa kunyamazishwa

Ni theluji tu. Wakati baridi likiwapiga idadi kubwa ya watu wa Afghanistan wenye njaa, theluji yenye muonekano wa binadamu inaonekana inaleta furaha kwenye kona moja ndogo ya mji wa Kabul.

Kundi la wasichana lilikuwa limesimama karibu na theruji kubwa kupiga picha za 'selfies'. Penigne wangekuwa mahala pengine kuliko hapa wanapoendelea kucheza na simu zao.


Mara wapiganaji watatu wa Taliban waliwaona. Wakasogea karibu - wanawake wale walikimbia. Akiwa na tabasamu, mmoja alielekea kwenye lile bonge la thaluji lenye muonekano wa binadamu - ambayo hutengenezwa kwa muundo wa binadamu wakati mwingine huwekwa mikono ya mbao na hata huvalishwa mavazi yanayoganda kwa barafu…alidhani haikuwa ya Kiislamu. Alirarua mikono ya fimbo, aliondoa kwa makini macho ya jiwe kwenye tharuji hiyo, pamoja na pua pia. Hatimaye, kichwa cha cha theruji hiyo.


Nilitaka kusikia kutoka kwa wanawake wenyewe. Wengi wako mafichoni, wote wanaogopa hatma zao na wengine kwa maisha yao. Bado kuna wanawake katika mitaa ya Kabul, wengine bado wakiwa wamevalia mavazi ya magharibi na kufunika vichwa vyao, lakini uhuru wao unaminywa - uhuru wa kufanya kazi, kusoma, kutembea kwa uhuru na kuishi uhuru.

Nilikutana na wanawake ambao wamelazimishwa kukukubaliana nan a kuingi katika vivuli vya Afghanistan mpya, ambao walichukua tahadhari kubwa wakati wakitoa maoni yao kwa uhuru. Wangeweza tu kufanya hivyo bila kujulikana - isipokuwa kwa Fatima, ambaye alisisitiza kuonyesha uso wake.

Wataliban wameharibu maisha ya Fatima mara mbili. Mara ya mwisho walipotawala Afghanistan, alilazimishwa kuingia kwenye ndoa akiwa na umri wa miaka 14 na hapo ukawa kikomo cha masomo yake aliyolazimika kuyakatiza ghafla.

Wakati huu, akiwa mkunga mwenye umri wa miaka 44 anaweza kusema ana kazi, lakini kama wanawake ilivyo kwa wanawake wengi, maisha ya kila siku yamebadilika yakiendelea kudorora.

'ninawaomba kwa unyenyekevu Taliban wasiingilie haki za wanawake katika elimu na ajira. Vinginevyo, ni sawa na kuondoa mkono mmoja (kiungo muhimu) katika jamii.

Amemaliza shahada yake miaka miwili iliyopita - lakini anakabiliwa na kikwazo kingine.

"Ilikuwa vigumu kwa msichana kupata elimu nchini Afghanistan, fikiria jinsi ilivyokuwa vigumu kwa mke mtu mzima kuajiriwa." Lakini Fatima alifanikiwa na tangu wakati huo amesaidia kuzalisha maelfu ya watoto.

Fatima anaonekana kukubali kwamba udhibiti wa Taliban unaweza kuwa wa kudumu, lakini ana matumaini wakati huu, wanaweza wakatawala kwa namna tofauti.


Huyu ni afisa usalama mwenye umri wa miaka 29, kujirembo saluni ni suala dogo asilolitilia maanani. Anasema kuwa anaogopa maisha yake.

Mnamo 15 Agosti, alianza siku hiyo kwa kutembelea nyumba salama inayomilikiwa na Kurugenzi ya Taifa ya Usalama (NDS), kitengo cha huduma za ujasusi ya Afghanistan.

Mikoa kwa mikoa ilipokuwa inaangua mikoni mwa Taliban, alikua anatembea usiku na mchana, kusaidia kuwarejesha maafisa katika kile alichodhani kuwa usalama wa Kabul.

Huko aliwapa pesa na kulipa gharama zao, kabla ya kuelekea makao makuu ya NDS kwenye barabara ya kuelekea uwanja wa ndege wa Kabul.

'Niliweza kusaidia maafisa wa NDS 100 kutoka maeneo mbalimbali kote nchini. Sikuamini kwamba Kabul ingeangukia mikononi mwa Taliban," alisema. Na hakuamini kwamba wangeweza kuvamia NDS na kuvamia mpaka Ikulu.

Ilibidi akimbie kuokoa maisha yake. Kundi la Taliban lilimska nyumbani kwake lakini tayari alikuwa ameondoka kwa kuhofia maisha yake.

Kundi la Taliban linasema lilichukua gari lake na bunduki ambayo alikuwa ameiacha nyumbani.

"Kitu kikubwa kwa mtu katika jeshi ni silaha. Ni uchungu sana kwetu wakati gaidi anapokuja na kukunyang'anya silaha."

Anamalizia kwa ombi la mwisho kwa Marekani na Uingereza: "Ulimwengu na jumuiya ya kimataifa kamwe isisahau kujitolea kwetu, juhudi zetu na mapambano yetu dhidi ya Taliban. Na bila kusahau ukweli kwamba tuliunda serikali katika kipindi cha miaka 20 iliyopita."

Mina ni binti mwenye akili, baada ya kumaliza kwenye nafasi za katika mitihani ya kitaifa ya Afghanistan ya "Kankur", ambayo kawaida kati ya wanafunzi 300,000 wanaomba nafasi ni 50,000 hufanikiwa kuingia katika chuo kikuu. Baada ya miaka minne ya masomo, ulisalia mwezi mmoja tu kuhitimu, ndipo Taliban walipovamia.

Anasema kuwa "katika masaa machache" mustakabali wa maisha yake ulibadilika. Hakutakuwa na diploma ya chuo kikuu kwa sasa. Mina alikuwa na matumaini ya kuwa mwanadiplomasia kama wengine katika familia yake, na labda kusoma katika chuo cha Oxford. Lakini kutumikia Afghanistan daima itakuwa kipaumbele.

"Bila elimu yetu, kazi zetu pia zinatiliwa shaka na mashaka. Hatuna matarajio mazuri kwa mustakabali wetu," anasema.

Bado anawasemea marafiki zake, lakini zaidi kupitia programu za mazungumzo kwenye simu yake.

Na hakati tamaa. Hata alipokaa kuzungumza na muandishi wa Makala haya katika chumba chenye giza, na utambulisho wake umefichwa, anasema anatarajia kutonyamazishwa.

"Nataka kutumikia nchi yangu na kuzungumza kwa haki za jinsia yangu. Nataka kupigania haki zangu, haki za kizazi changu," anasema. "Nadhani ni furaha kupigania haki zetu, kupigania familia yangu, wenzangu na marafiki zangu. Nina uwezo wa kupaza sauti."

Zahra, 34 anasema kutokana na hofu zilizopo nchini humo, watoto wake wanasema wanatamani wazazi wao wasingehudumu katika vikosi vya usalama.

"Ninawaambia ni sawa na natumai siku moja watajua kwamba tumetoa huduma kubwa kwa kutoa sadaka maisha yetu, kujiweka katika hatari kubwa na bado wako tayari kutumikia. Kwa hivyo nasubiri siku hiyo ifike."

Anaongeza, "Marekani na NATO zilitutia moyo kuchukua kazi hizi. Tulipewa mafunzo ya pamoja tukiwa wanawake wengi kutoka Marekani, Canada, Ujerumani, Uholanzi, Poland na nchi nyingine nyingi.

Walisema watasimama pamoja nasi - bega kwa bega - lakini mwishowe wametuacha peke yetu, tumetelekezwa."

Mbali na Fatima, majina ya wanawake tuliozungumza nao yamebadilishwa ili kulinda utambulisho wao.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii