UN Yalaani Mauaji ya Raia Kaskazini mwa Sudan Kusini

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa raia kadhaa wamepoteza maisha kufuatia machafuko mapya yaliyozuka Kaskazini mwa Sudan Kusini ndani ya saa 48 zilizopita.

Kupitia Ujumbe wake nchini humo (UNMISS), Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa unatiwa wasiwasi na kuongezeka kwa vitendo vya vurugu katika eneo la Abiemnom, lililopo karibu na mpaka wa Sudan.

Aidha kwa mujibu wa taarifa hizo, kundi la vijana wenye silaha lilivamia makao makuu ya Kaunti ya Abiemnom na kuwashambulia wananchi bila kuchagua, hali iliyosababisha vifo na taharuki kubwa miongoni mwa wakazi.

Hata hivyo UNMISS imesisitiza umuhimu wa kulindwa kwa raia na kuitaka pande husika kuchukua hatua za haraka kurejesha usalama na utulivu katika eneo hilo.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii