Dkt Samia: Tutajiepusha na Athari za Kupanda Bei ya Mafuta

Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imejipanga kuimarisha usalama wa nishati ya mafuta ili kulinda uchumi dhidi ya athari za kupanda kwa bei katika soko la dunia.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo, Jumanne Machi 3, 2026, wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa matenki ya kupokea mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam.

Amesema mradi huo utaongeza uwezo wa Taifa kuhifadhi mafuta kwa akiba ya kimkakati, hatua itakayosaidia kupunguza athari za misukosuko ya kimataifa inayoathiri bei ya nishati hiyo.

“Misukosuko iliyotokea wiki iliyopita na tunayoendelea nayo tayari imeshapandisha bei ya mafuta kwa asilimia 13 mpaka jana. Sasa hatujui leo na siku zinazokwenda, lakini tumuombe Mungu watu wale wakae juu ya meza wazungumze wakubaliane ili misukosuko iishe,” amesema Rais Samia.

Hata hivyo ameeleza kuwa uwekezaji huo ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa kuhakikisha nchi inakuwa na uhakika wa upatikanaji wa mafuta na utulivu wa bei kwa wananchi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii