Hezbollah yazishambulia kambi za kijeshi za Israel

Kundi la Hezbollah limethibitisha kuzilenga kambi tatu za kijeshi za Israel katika mashambulizi ya kulipiza kisasi baada ya miundo mbinu yake kushambuliwa na Israel nchini Lebanon.

Taarifa ya wanamgambo hao imesema imeilenga  kambi ya jeshi la anga ya Ramat David na kambi ya Meron kaskazini mwa Israel.

Wakati huohuo, jeshi la Israel limeeleza kuwa limevipeleka vikosi vya ziada kusini mwa Lebanon usiku wa kuamkia Jumanne kama hatua ya kuwalinda raia wake na kuzuia mashambulizi ya Hezbollah.

Kulingana na Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz serikali imechukua hatua hiyo baada ya Hezbollah kurusha makombora yaliyoilenga Israel siku ya Jumapili.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii