Ndege ya Cristiano Ronaldo Yaondoka Ghafla

Ndege binafsi ya kifahari ya thamani ya pauni milioni 61 inayomilikiwa na nyota wa soka Cristiano Ronaldo imeripotiwa kuondoka Saudi Arabia kuelekea Madrid usiku wa kuamkia leo Machi 3, 2026 wakati hali ya usalama ikiendelea kuwa tete mjini Riyadh.

Ronaldo, mwenye umri wa miaka 41, anaishi katika mji mkuu huo wa Saudi pamoja na mpenzi wake, Georgina Rodriguez, na watoto wao watano. Hata hivyo, bado haijathibitishwa kama familia hiyo ilikuwa ndani ya ndege hiyo wakati ilipoondoka.

Tukio hilo limekuja baada ya mashambulizi mawili ya ndege zisizo na rubani kupiga Ubalozi wa Marekani katika mjini wa Riyadh, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Iran.

Wakati huohuo, ripoti zimedai kuwa jengo la wafanyakazi wa Marekani nchini Bahrain liliharibiwa.

Taarifa hizo zimezua taharuki katika eneo la Mashariki ya Kati, huku raia wa kigeni wakiripotiwa kuondoka kwa maelfu kadhaa kadri mzozo huo unavyoingia siku ya nne.

Kwa sasa, haijulikani iwapo kuondoka kwa ndege ya Ronaldo kunahusiana moja kwa moja na hali ya usalama, lakini tukio hilo limeibua mjadala mkubwa mtandaoni.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii