Msanii wa muziki wa RnB kutoka nchini Kenya, Bridget Blue, ameendelea kuthibitisha ubora wake katika tasnia ya muziki baada ya kuachia albamu yake mpya aliyoipa jina la “RNB”. Albamu hiyo imepokelewa vizuri na mashabiki wake, huku ikionesha ukuaji wake mkubwa kisanaa pamoja na ubunifu katika muziki wa RnB.
Katika albamu hiyo, Bridget Blue amewashirikisha wasanii wawili pekee, akiwemo Nikita Kering na Bien, jambo linaloonesha kuwa alilenga zaidi ubora kuliko wingi wa kolabo
Miongoni mwa nyimbo hizo ni “Mimi na Wewe” aliyomshirikisha Nikita Kering. Akizungumzia kolabo hiyo, Bridget Blue alieleza kuwa wana ukaribu mkubwa sana kama marafiki, na ukaribu huo ndio uliowapa msukumo wa kuandika na kurekodi wimbo huo, ambao ni maalum kwa ajili ya kusherehekea urafiki wa kweli na uhusiano wa karibu.Kwa ujumla, albamu ya “RNB” inaonyesha uwezo wa Bridget Blue kujisimamia kisanii pamoja na kufanya chaguo sahihi la ushirikiano, huku akiwapa mashabiki wake kazi yenye ubora, ujumbe mzuri na burudani ya hali ya juu.