Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amemkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, kwa ajili ya kuanza mbio zake wilayani humo na kuzindua miradi ya maendeleo.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo Aprili 13, 2026 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, ambapo mwenge huo umetokea Kaskazini Unguja, Zanzibar. Katika mzunguko wake, Mwenge wa Uhuru utakagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi 35 yenye thamani ya shilingi bilioni 113.5 katika wilaya zote tano za jiji hilo.
Ratiba inaonesha kuwa baada ya Ilala, Mwenge utaelekea Kigamboni, kisha Temeke, Ubungo na Kinondoni kabla ya kukabidhiwa Mkoa wa Pwani Aprili 18, 2026.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime