Papa Leo XIV anaanza ziara ya siku 10 barani Afrika

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIV anaanza ziara ya siku 10 barani Afrika itakayomfikisha katika mataifa manne.

Anabeba ujumbe wa kuwahimiza viongozi duniani kusaidia kushughulikia mahitaji ya bara hilo wanakoishi zaidi ya asilimia 20 ya wakatoliki wote duniani.

Kituo cha kwanza cha ziara ya kiongozi huyo wa kiroho itakuwa ni nchini Algeria na baadaye ataelekea Cameroon kisha Angola na kuhitimisha nchini Guinea ya Ikweta.

Taarifa ya Makao Makuu ya Kanisa Katoliki mjini Vatican imesema Papa Leo XIVanatumai ziara yake "itasaidia kuelekeza macho ya ulimwengu barani Afrika" eneo ambalo bado linakabiliwa na changamoto lukuki.

Amepangiwa kwa jumla kuitembelea miji 11 kwenye nchi hizo nne katika kile kinachozingatiwa kuwa mojawapo ya safari ngumu kuwahi kufanywa na Baba Mtakatifu kwa miongo kadhaa iliyopita.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii