Rais wa Marekani, Donald Trump, amemkosoa vikali kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Pope Leo XIV, akimtuhumu kuwa na msimamo unaoonekana kuipa nafasi Iran kumiliki silaha za nyuklia.
Kauli hiyo imekuja kufuatia Papa huyo kuendelea kupinga vita vinavyoendelea kati ya Marekani, Israel na Iran, huku akisisitiza umuhimu wa amani na kupinga matumizi ya nguvu pamoja na kuenea kwa silaha za nyuklia.
Kupitia mitandao ya kijamii, Trump alimueleza Papa kama dhaifu katika masuala ya usalama na sera za nje, akisisitiza kutoridhishwa na msimamo wake.
Hata hivyo, Papa Leo XIV ameendelea kusisitiza kuwa suluhisho la kudumu ni mazungumzo ya amani, akieleza kuwa dini haipaswi kuunga mkono migogoro.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime