Watoto wanane wauawa katika shambulizi Louisiana

Mwanamume mmoja amewauwa watoto wanane, saba ambao wakiwa wake mwenyewe na kuwapiga risasi wanawake wawili katika shambulizi moja mjini Shreveport, jimboni Louisiana nchini Marekani.

Kulingana na taarifa za polisi mwaka 2019 bwana huyo alikabiliwa na kesi ya kupatikana na bunduki kinyume na sheria.

Kwa wakati huu amekuwa katika mchakato wa kuachana na mke wake na walitarajiwa kuwa mahakamani leo Jumatatu.

Kulingana na majirani, mashambulizi hayo yalitokea wakati walipokuwa wakizozana na mke wake kuhusu kutengana kwao.

Katika mkutano na waandishi wa habari nje ya nyumba moja yalikotokea mauaji hayo, meya wa mji huo Tom Arceneaux, amesema hali hiyo ni ya kusikitisha na tukio baya zaidi kuwahi kushuhudiwa ametoa wito wa utulivu na maombi kwa jamii ya eneo hilo.

Hata hivyo mauaji hayo yametajwa kuwa mabaya zaidi tangu januari mwaka 2024 wakati watu 8 walipouawa mjini Chicago.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii