Ni rasmi ndoa ya Kardashian na Ye {Kanye West} imevunjika

Kim Kardashian hatimaye ametalakiana na mume wake Ye aliyejulikana kama Kanye West baada ya ndoa ya miaka minane .

Katika uamuzi wa mahakama uliotolewa kupitia njia ya video nyota huyo pia aliliondoa jina la West kutoka katika jina lake la mwisho.

Kardashian , ambaye aliwasilisha ombi la talak ana rappa huyo mwaka uliopita, aliiomba mahakama kuachika ramsi mwezi Disemba.

Hatahivyo wawili hao sasa watalazimika kusuluhisha ugavi wa mali na uleaji wa Watoto wao wanne.

Uamuzi huo wa siku ya jumatano - uliompatia kardashian ruhusa ya kuachika - una maana kwamba talaka hiyo itafanyika mara mbili: kwanza kundoa jina lake , kutalakiana kindoa na pili ugavi wa mali na jinsi watakabyowalea Watoto wao.

Katika taarifa kadhaa za kiapo zilizowasilishwa manmo mwezi Disema, nyota huyo mwenye umri wa miaka 41 alisema kwamba alipendelea ndoa hiyo kufikia ukingoni.

"Ninaamini kwamba mahakama ikifutilia mbali ndoa yetu itamsaidia Kanye kukubali kuwa uhusiano wetu wa ndoa umekwisha," aliandika katika taarifa yake mwezi uliopita.

Ye, 44, ambaye hakuwepo kwenye kikao hicho, alikuwa amepinga hadharani kutengana na akaomba Kardashian arejee kwenye ndoa yao.

Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo siku ya Jumatano, wakili wa Ye alisisitiza makubaliano kutoka kwa Kardashian ili kuondoa mipango yoyote ya ndoa ambayo anaweza kuwa nayo na mtu yeyote..

Kardashian na wakili wake waliitjaa hatua hiyo "isiyo na kifani" na ikakataliwa na jaji.

Wawili hao walianza kuchumbiana mnamo 2012 na kufunga ndoa miaka miwili baadaye.

Ye ni mojawapo ya majina makubwa katika muziki wa rap, duniani kupitia vibao kama vile Stronger, Jesus Walks na Gold Digger. Pia amepata mafanikio kama mbunifu wa mitindo

Kardashian alipata umaarufu kwa mara ya kwanza mwaka wa 2007 kama nyota wa kipindi cha TV kuhusu familia yake, Keeping Up With The Kardashians, na tangu wakati huo amezindua chapa za mitindo na urembo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii