Milio ya risasi imesikika pia
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Modibo Keita kwenye mji mkuu Bamako huku
mashuhuda wakisema kuwa wameshuhudia pia mapigano kwenye mji wa kaskazini wa
Gao na Sevaré ulio katikati ya Mali.
Nchi hiyo imekuwa ikikabiliwa na mashambulizi yanayofanywa na
makundi ya wanamgambo wenye itikadi kali yanayohusishwa na al-Qaeda na kundi
linalojiita Dola la Kiislamu.
Aidha baada ya taarifa za mashambulizi hayo, jeshi limetangaza kuwa
linapambana na makundi ya kigaidi ambayo yameshambulia maeneo kadhaa ya mji
mkuu na mengine ndani ya nchi hiyo
Hata hivyo mji wa Mali,kando ya kitisho cha makundi ya itikadi kali, ina historia ndefu ya uasi unaoongozwa na jamii ya Watuareg kaskazini mwa nchi inayoongozwa na utawala wa kijeshi ulioingia madarakani baada ya mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2020 na 2021.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime