Janga hilo lilitokea nje ya pwani ya Djibouti. Angalau wahamiaji 139 wamefariki na zaidi ya wengine 84 hawajulikani walipo baada ya boti yao kuzama usiku wa Oktoba 8 kuamkia Oktoba 9, Umoja wa Mataifa umesema leo Jumapili, Oktoba 11.
Watu 109, wakiwemo watoto 15, wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 116 hawajulikani walipo baada ya boti yao kuzama karibu na eneo la Guhere, kaskazini mwa mji wa Obock nchini Djibouti, usiku wa kuamkia Oktoba 8 hadi 9, 2026.
Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) kupitia Umoja wa Mataifa (UN) limeripoti kuwa boti hiyo ilikuwa imebeba takriban wahamiaji 305 hadi 350 waliokuwa wakisafiri kutoka Djibouti kwenda nchini Yemen. Timu za uokoaji na za dharura zipo kazini kusaidia manusura walionusurika.
Manusura waliripoti kwamba boti hiyo ilikuwa imebeba karibu watu 350 kutoka Djibouti kwenda Yemen. Ilizama nje ya pwani ya mji wa Obock nchini Djibouti. Kulingana na mkuu wa ujumbe wake nchini Djibouti, Alexandre Coissac, "Ni pigo kubwa na la kusikitisha kwa kupoteza raia wengi hivo."
Ripoti ya awali ilionyesha angalau watu 109 wamefariki na 116 hawajulikani walipo. IOM ilirekebisha takwimu hii saa chache baadaye: "Idadi ya vifo 109 imeongezeka baada ya kugunduliwa kwa miili 30 zaidi." Hii bado ni idadi ya muda, kwani "shughuli za utafutaji na uokoaji zinaendelea."
Waathiriwa wote walikuwa raia wa Ethiopia. Kila mwaka, mamia ya maelfu ya watu huondoka Ethiopia kusafiri Njia ya Uhamiaji ya Mashariki, moja ya njia zenye shughuli nyingi zaidi duniani. Wakikabiliwa na ugumu wa kiuchumi, watu hawa wanatumaini kupata fursa katika nchi za Ghuba, haswa Saudi Arabia, na mzozo nchini Yemen—ambao kwa sasa unaongezeka tena—hauwazuii kuondoka.
Wahamiaji wanavuka maeneo ya jangwa ya Djibouti, ambapo halijoto tayari ni kali, kabla ya kukabiliwa na hatari za mzozo kati ya waasi wa Houthi na serikali ya Yemen.
Katika miezi mitatatu ya kwanza ya mwaka 2026, IOM ilirekodi vifo 94 katika njia hii ya uhamiaji, takwimu ambazo shirika hilo linaamini ni za chini sana. Kwenye takwimu hizi, sasa vinasajiliwa pia vifo vilivyoripotiwa leo Jumapili, tarehe 11 Oktoba.