Rais mstaafu wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila amechukua usukani wa harakati mpya ya kisiasa na kijeshi inayofahamika kama Front for the Refoundation of the Nation, FRN
Tangazo la kuanzishwa kwa Harakati mpya hili la FRN lilitolewa Jumatatu jioni, Oktoba 12, 2026, huko Goma, ambapo Jukwaa hili jipya sasa linajumuisha Muungano wa (AFC) na kundi la waasi wa (M23).
Rais huyo wa zamani wa Kongo, mkosoaji mkubwa wa Félix Tshisekedi, ndiye Kiongozi wa FRN akiwa amezungukwa na makamu wa rais watatu, akiwemo Corneille Nangaa, Bertrand Bisimwa, na Sultani Makenga, ambao hapo awali walikuwa wanachama wa ngazi za juu wa AFC-M23, Watatu hawa wako chini ya vikwazo vya kimataifa kufuatia jukumu lao katika mzozo mashariki mwa Kongo,huku Dokta Freddy kaniki ametajwa kama katibu mkuu na mtendaji atakayeshughulikia masuala ya uratibu.
Tamko hilo lilisomwa na Claude Ibalanky, balozi na mshauri wa zamani wa Rais wa sasa Felix Tshisekedi, Akishutumu utawala wa kinshasa kwa kuingiza nchi hatarini, na kuashiria Kifungu cha 64 cha Katiba—ambacho kinasema kila raia wa Kongo ana wajibu wa kumpinga mtu yeyote au kikundi kinachochukua madaraka kwa nguvu au kuyatumia kinyume cha Katiba.
Tangazo hilo limekuja siku chache baada ya hotuba ya rais mstaafu huyo Joseph kabila, aliyoitoa siku ya Ijumaa usiku, ambayo alisema anataka kuchukua hatua kukabiliana na kile alichokieleza kwamba nchi hiyo ipo hatarini, chini ya rais aliyerithi madaraka kutoka kwake Félix Tshisekedi tangu kushika hatamu za uongozi mwaka 2019
Mwaka mmoja baada ya kuhukumiwa kifo na Kinshasa kwa "uhaini" na kushirikiana na AFC M23, Joseph Kabila ametangaza rasmi nafasi yake katika uasi, katika Kile Kinshasa ililaumu tangu hapo awali. Serikali ya Kinshasa bado haijatoa tamko lolote kuhusiana na taarifa hii.