Msako wafanyika katika makaazi ya mbunge Ilhan Omar

Nchini Marekani, Maofisa wa usalama wamefanya msako katika nyumba ya mbunge wa chama cha Democratic, Ilhan Omar, jijini Washington DC.

Ofisi ya Mbunge huyo imetaja hatua hiyo kama juhudi za utawala wa Rais Donald Trump kuwahangaisha wapinzani wake.

Msako huo umefanyika ikiwa imesalia majumaa kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa wa wabunge wa Novemba 3 nchini Marekani.

Katika uchaguzi huo, chama cha Rais wa Marekani Donald Trump kitakuwa kinalenga kuendelea kudhibiti bunge la Congress.

Inaripoptiwa kuwa maofisa hao wa usalama waliondoka kwenye makaazi ya mbunge huyo na baadhi ya bidhaa zisizojulikana.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa, huenda msako huo unahusishwa na tuhuma kuwa marehemu baba ya mbunge huyo alishiriki udaganyifu wakati akiwasilisha makaratasi yake ya uhamiaji mbunge huyo alipokuwa angali mdogo. Hakuna kesi iliowasilishwa mahakamani dhidi ya madai haya.

Rais Trump amekanusha kuwa nyuma ya msako huo lakini amesisitiza kwamba mbunge huyo ni mtu mkorofi.

Omar, ambaye alizaliwa nchini Somalia, alienda Marekani akiwa kama mkimbizi wakati akiwa mtoto kabla ya kupewa uraia wa Marekani kupitia njia za kisheria.

Amekuwa akilengwa na Rais Trump mara kwa mara, mashambulio yanayohusishwa na uhamiaji.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii