Rais wa Marekani Donald Trump amesisitiza kwamba Urusi na Ukraine zimekubaliana kusitisha mashambulio dhidi ya miundombini ya nishati, akizitaka pande hizo kusitisha vita vinavyoendelea.
Matamshi ya Trump yamejiri wakati huu Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akiituhumu Urusi kwa kushambulia miundombinu sita ya nishati nchini mwake tangu Rais Trump atangaze makubaliano hayo Jumapili iliopita.
Trump amedai kuwa vita hivyo viliovyozuka mwezi Februari mwaka wa 2022 vimesababisha vifo vya karibia watu Elfu 32 mwezi huu peke.
“Ninachofahamu ni kwamba Zelenskyy na Putin wamekubali kuungana na kumaliza vita hivi,” Amesema Trump.
Trump wikendi iliopita, alitangaza kuwa Ukraine na Urusi zilikuwa zimekubaliana kusitisha mashambulio dhidi ya miundombinu ya nishati kwenye nchi zao.
Tangazo hilo lilipingwa vikali na Rais Zelenskyy aliyedai kuwa makubaliano hayo yanarejesha nyuma juhudi zilizopigwa na mataifa ya Magharibi kuitenga Urusi kiuchumi na ni kama Zawadi kwa Putin.