Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Leo XIV amekutana na manusura sita wa unyanyasaji wa kingono unaohusishwa na makasisi mjini Madrid na kuahidi kuzingatia mapendekezo yao kuhusu jinsi Kanisa linavyoweza kuboresha majibu yake kwa kashfa hiyo.
Vatican imesema mkutano huo ulidumu takribani saa moja na uliwaleta pamoja manusura waliotoa ushuhuda wao pamoja na mapendekezo ya mageuzi ndani ya Kanisa Katoliki.
Nchini Uhispania kashfa ya unyanyasaji wa makasisi imeibua mjadala mkubwa baada ya ripoti mbalimbali kuonyesha uwezekano wa maelfu ya waathirika, huku Kanisa likikiri kuwepo kwa mamia ya wahusika tangu mwaka 1945.
Papa Leo amesisitiza umuhimu wa kusikiliza waathirika haki,fidia na ulinzi bora akisema Kanisa linapaswa kuwa mahali salama pa uponyaji na faraja.
"Katika jamii zetu leo hii, bado kuna pingamizi nyingi ambazo hazijengi bali zinatenganisha na kuwafanya watu wajihisi upweke na wakati mwingine kwa kuhofia kwamba tutalazimika kukabiliana na mambo tusiyoyapenda pale tutakapoamua kuzibomoa kuta hizo za pingamizi ndio maana tunachagua kuendelea kuzifumbia macho kama hazipo na hivyo kuendelea kuziimarisha na mara nyingi huwa tunazipuuza kabisa.”
Hata hivyo baadhi ya makundi ya waathirika yamelalamikia kutengwa katika mkutano huo, huku Vatican ikisisitiza kuwa mazungumzo yanaendelea katika ngazi mbalimbali.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime