Nchini Nigeria, maafisa wa usalama wamekabidhi kwa serikali wanawake na watoto 400 waliokolewa mikononi mwa wanajihadi wa Boko Haram.
Watu hao kwa sasa wamepewa hifadhi ya muda, katika jimbo la Borno, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo baada ya kuokolewa.
Hatua hii imekuja baada ya wanajeshi kuripoti kuwa, ilikuwa iliwaokoa mateka 360 mwishoni mwa wiki iliyopita, na wnegine 82 wiki tatu zilizopita.
Baada ya kutekwa ripoti zinasema, waliplekewa katika milima ya Gwoza, Kilomita 10 kutoka katika mpaka wa Nigeria na Cameroon , kabla ya kuokolewa.
Watekaji walitaka Mamilioni ya Naira, kama kikombozi kabla ya kuwaachia huru mateka hao, lakini serikali ya Nigeria inasema, haikuwahi kutoa fedha hizo.
Wakati hayo yakijiri, watu wengine 39 wametekwa katika kijiji cha Magamin Diddi katika jimbo la Zamfara.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime