Mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, Karim Khan, amesimamishwa kazi kufuatia kesi za kinidhamu zilizoanzishwa baada ya madai ya unyanyasaji wa kingono kuwasilishwa dhidi yake.
Baraza la Mahakama ya Kimataifa ya Jinai limetangaza uamuzi huo siku ya Jumatatu jioni, baada ya kamati yake ya utendaji kupiga kura ya kuipeleka kesi ya Bw. Khan kwenye kikao maalum cha nchi wanachama ili kuzingatia mustakabali wake.
Kulingana na hati iliyoonekana na Gazeti la The Guardian, kamati hiyo, inayoundwa na nchi 21 wanachama wa Mahakama hiyo, ilipiga kura kwa wingi kuhitimisha kwamba Bw. Khan alifanya utovu wa nidhamu mkubwa kuhusiana na madai ya unyanyasaji wa kingono.
Khan, wakili maarufu wa Uingereza, amekanusha mara kwa mara madai hayo yaliyoibuka kwa mara ya kwanza mwaka wa 2024.
Karim Khan, wakili maarufu wa Uingereza, amekanusha mara kwa mara madai yaliyoibuka mwaka wa 2024 na kusababisha msukosuko wakati wa uongozi wake kama mkuu wa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC). Madai haya yalitolewa na mwanamke aliyefanya kazi chini uongozi wake katika makao makuu ya Mahakama huko The Hague.
Mwendesha Mashtaka wa ICC anadaiwa kujaribu kuficha mashtaka ya utovu wa nidhamu wa kingono dhidi yake
Uamuzi wa kuipeleka kesi hiyo kwa nchi 125 wanachama wa ICC ni hatua isiyo ya kawaida kwa Mahakama Kuu na inaweza kusababisha kura ya kufutwa kwa mwendesha mashtaka.
Kura ya kamati hiyo ni maendeleo ya hivi karibuni katika kesi ambayo imeitikisa ICC kwa karibu miaka miwili.
Madai yaliyotolewa na mfanyakazi wa ICC yanahusu mwenendo wa Khan kati ya mwaka 2023 na 2024. Anamtuhumu kwa kujihusisha na tabia ya ngono ya kulazimisha na isiyo ya ridhaa kwa muda mrefu. Vitendo hivi vinavyodaiwa vilitokea katika vyumba vya hoteli wakati wa safari za kikazi, ofisini kwa Khan, na nyumbani kwake.
Mawakili wa Khan hapo awali walisema kwamba "anakanusha kabisa" kuwa "amemnyanyasa au kumtendea vibaya mtu yeyote, kutumia vibaya nafasi au mamlaka yake, au kujihusisha na tabia ambayo inaweza kutafsiriwa kama ya kulazimisha, ya matusi, au isiyofaa kitaaluma."
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime